Jumanne, 12 Mei 2015

TEKNOLOJIA YA GOLI YAIMALIZA ARSENAL NYUMBANI

WACHEZAJI WA ARSENAL WAKIJISHIKA KICHWA

Goli la dakika ya 85 la mshambuliaji aliyetokea benchi wa Swansea Bafetimbi Gomis liliiwezesha Swansea kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Arsenal katika uwanja wa Emirates.
Mpira wa krosi toka kwa winga wa Swansea Jeffeson Montero ulimkuta Gomis ambaye aliunganisha kwa kichwa na kwa haraka sana kipa wa Arsenal David Ospina alijitahidi kuokoa lakini mpira ulishavuka mstari huku mchezaji pekee aliyeshtukia hilo akiwa ni Gomis ambaye alinyosha mikono kuonyesha kuwa ni goli na Refa kwa kutumia saa yake alipata ujumbe kuwa ni goli na kuamuru mpira ukaanzwe katikati.
Gomis aliingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Ki Sung Young mabadiliko ambayo yalileta faida kwa Swansea ambayo inakua timu ya pili kuifunga Arsenal katika uwanja wa Emirates katika mechi za ligi kuu timu nyingine ikiwa ni Man United. Kwa Matokeo hayo Arsenal wanabaki katika nafasi ya 3 wakiwa na pointi 70 pointi 3 nyuma ya Man City wanaokamata nafasi ya 2 na pointi mbili zaidi ya Man United wanaokamata nafasi ya 4. Swansea wao wako katika nafasi ya 8