Jumapili, 28 Juni 2015

Mtangazaji maarufu Hamis Dambaya atangaza kugombea ubunge Kibiti

Mtangazaji maarufu Hamisi Dambaya, amesema anakusudia kugombe ubunge wa Jimbo la Kibiti kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM).
Dambaya ambaye pia ni mchambuzi wa masuala ya siasa alitangaza nia hiyo wakati akiongea katika kipindi cha “Jicho Letu Ndani ya Habari” cha Star Tv.
Pia amedai anamshukuru Rais Kikwete kwa kumteua mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba.
“Namshukuru Rais Kikwete kwani uteuzi wake ulinipa uzoefu na hivyo kama nitafanikiwa kuingia bungeni sitokwenda kujifunza, bali nitakwenda kufanya kazi,” alisema Dambaya.
Dambaya amekuwa akifanya kazi muda mrefu katika Televisheni ya Mlimani (Mlimani Tv) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Aliwahi kuwa mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba akiwakilisha tabaka la wakulima.
Hamis Dambaya aliingia CCM Chipukizi mwaka 1983.