Jumapili, 3 Mei 2015

YANGA OUT YAPIGWA KADUCHU NA ETOIL DU SAHEIL


Mabingwa wa ligi kuu ya Tanzania bara yanga sc jana usiku imetolewa katika michuano ya kimataifa baada ya kukubali kichapo cha goli 1-0 toka kwa Etoil Du Saheil na kupelekea kutolewa kwa jumla ya goli 2-1.

Katika mchezo wa jana uliochezwa nchini Tunisia Etoil Du Saheil waliuwanza mchezo kwa kasi na kupelekea yanga sc kukaa nyuma na kuzuia mashambulizi ya Etoil katika dakika tano za mwanzo, ambapo baada ya dakika hizo yanga sc nao walianza kujibu mashambulizi.
Etoil Du Saheil waliandika goli la kuongoza katika dakika ya 24 kupitia kwa Ammar Jemal aliyeunga kwa kichwa krosi ya Alkhali Banguora, goli lililodumu dakika zote za mchezo.

Katika dakika ya 34 Mchezaji wa Etoil alizawadiwa kadi nyekundu na kupelekea wamalize wakiwa pungufu kwa mchezaji mmoja, ambapo kuilpelekea yanga SC kutawala mchezo huo kwa dakika zilizo salia.

Mchezaji huyo wa Etoil alizawadiwa kadi ya pili ya njano baada ya kumchezea vibaya Saimon Msuva na kupewa kadi nyekundu.

Katika kipindi cha pili Etoil walitumia muda mwingi kuzima mashambulizi ya yanga huku wao wakipeleka mashambulizi ya kushtukiza ambapo hakuzaa goli la aina yoyote ile katika kipindi hicho cha pili na kupelekea mchezo kumalizika kwa Etoil kuibuka na ushindi wa goli 1-0.

Kwa matokeo hayo ya jana na yale ya uwanja wa taifa wiki mbili zilizopita, kuna pelekea yanga kutolewa kwa jumla ya goli 2-1.

Yanga sc jana: Deogratus Minushi, Juma Abdul, Oscar Joshua, Mbuyu Twite, Kelvin Yondani, Juma Said, Saimon Msuva, Salum Telela/Andrey Countinho, Amis Tambwe, Kpah Sherman/Juma Javu, Mrisho Ngassa