Alhamisi, 9 Julai 2015
Watangaza nia kupitia ubunge mbeya waendelea kupambana kila kona lakini je wataifanyia nini mbeya
Jiji la mbeya ni moja ya majiji makubwa hapa nchini tanzania na pilika zake za wafanyabiashara zinazidi kukua kila siku.majengo makubwa na ya kisasa yanaendelea kujengwa na wakazi wake lakini swali ninalojiuliza hawa wanasiasa wanaowania jimbo la mbeya mjini nini wanataka kuwafanyia wakazi wa mbeya nimeona wakiendelea kupiga siasa za chini chini katika maeneo mbalimbali ya jiji la mbeya .wengine wakiandaa michezo ya aina mbalimbali toka mwaka 2012,wengine wakienda makanisani na misikitini wakitoa misaada mbalimbali kwa sababu eti wataonekana viongozi wasafi.sasa mimi najiuliza kuna viwanda vingapi vimekufa hapa mkoani mbeya sijamsikia hata mmoja kuanzisha mkakati wa kwenda hata kule zana za kilimo (ZZK) kufufua kile kiwanda hata kusafisha tu lile eneo na kuongelea tatizo ilo kwa wananchi kimya sasa nnawafumbua macho muanze na ilo .hata aliye madarakani kwa sasa Mh joseph mbilinyi umejisahau mpaka kipindi kimefunga sijui utakuja kuwambia nini wana mbeya .siasa ya sasa sio ya jana inataka mikakati. nikirudi nyuma tu hapo juzi mnasema mnapenda michezo nyinyi wanasiasa wa mbeya uwanja wa sokoine ulikuwa unahitaji matengenezo mlipopitishiwa bakuli mlianza kulusha danadana ikawa shida .mpaka chama cha mpira mkoa (MREFA) na halmashauri ya jiji kupitia meya wa jiji Mh Atanas kapunga kufanya jitihada na watu wa magereza na wadau wa soka wakiwemo kampuni ya Ajim enterprises ltd waliosababisha uwanja ukatengenezwa kuwekwa magori na magari yake ya kampuni kuacha shughuli na kuanza kubeba nyasi toka tukuyu .sasa leo kwa sababu mnataka kitu na siasa chafu za kutaka kuwaonga wananchi kwa wali na vitenge kiukweli sio siasa ya leo.ushauri wangu watu wa mbeya wana matatizo mengi sana yakiwemo ya wafanyabiashara kutokuwa na sehemu za kudumu katika kufanyia biashara zao kunyanyaswa kwa wamachinga ,vibanda vyao kuvunjwa usiku wa manane ,watu wa bajaji kunyanyaswa na polisi wakati miundo mbinu ya mbeya ni mibovu ramani zake haziko sawa hii ni kazi ya nyinyi mnaotaka ubunge mkae na muangalie nikichaguliwa nitawafanyia nini wana mbeya .itaendelea wiki ijayo