Uongozi wa yanga ukiongozwa na katibu wake mkuu Jonas Tibohora jana ulifika mkoani mbeya majira ya saa mbili na nusu ukitokea jijini dar es salaam kwa ndege na kutua katika uwanja wa songwe uliopo mkoani mbeya na kuanza safari ya kuelekea wilayani mbozi na kufanya mazungumzo na uongozi na Kimondo fc .
Hata hivyo kikosi kazi cha Harubutz kilikwenda mpaka wilayani mbozi kutaka kujua nini kinachoendelea kati ya uongozi wa kimondo fc na yanga ,majibu yalipatikana baada ya masaa mawili pande zote kukubaliana.makubaliano yalikuwa kama yafuatavyo na kuwekeana makubaliano pande zote mbili Timu yanga imekubali ombi la timu ya kimondo fc la kutaka kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya kimondo fc wilayani mbozi na mapato yote yatakayoingia uwanjani yatakuwa ni timu ya kimondo fc kama makubaliano yalivyoafikiana pande zote mbili.hata hivyo mkurugenzi wa timu ya kimondo fc Elick Ambakisye alisema kwa sasa mkataba wa Geofrey Mwashiuya na klabu ya yanga huko huru na yanga wako tayari kumtumia mchezaji huyo popote pale.hata hivyo uongozi wa yanga bado upo wilayani mbozi kwa ajiri ya kumalidhana na mchezaji mwingine wa kimondo fc siku ya leo