Jumatatu, 15 Juni 2015

Taifa Stars hali dhoofu yalala 3-0 mbele ya Mafarao

Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars imekiona cha mtema kuni baada   kuchabangwa mabao 3-0 dhidi ya Misri katika mchezo wa kufuzu fainali za kombe la mataifa ya Afrika.
Mabao ya Misri yamewekwa kimiani na wachezaji Rabia katika dakika ya 60, Bassema dakika ya 65 na Salaha katika dakika ya 70.
Hata hivyo mlinda mlango wa Taifa Stars Deo Munishi (Dida) ndiye ameibuka nyota wa mchezo huo baada ya kuokoa hatari zilizokuwa zinaelekezwa langoni mwake kila muda.
Kwa matokeo hayo Tanzania  inaburuza mkia katika kundi G ambalo lina timu za Nigeria, Misri na Chad