WAZIRI
MKUU Mizengo Pinda ambaye pia ametangaza nia ya kuwania urais wa
Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) amepata wadhamini 2644
Akitoa
nasaha zake kwa wakazi hao leo (Jumatano, Juni 17, 2015), Waziri
Mkuu aliwashukuru wote waliomdhamini huku akiwaomba waendelee kumuombea
safari zote zilizo mbele yake na zoezi zima liende vizuri kwani suala
la urais siyo lelemama bali ni la kumtanguliza Mungu.
Akifafanua
zaidi, Waziri Mkuu Pinda alisema: “Suala la urais si la kufa na kupona
bali ni la kumtanguliza Mwenyezi Mungu kwanza. Kila mgombea anapaswa
amuombe Mungu kwamba kama itampendezea na kumuona anafaa ndipo amchague
yeye (mtangaza nia).”
“Ndiyo
maana mara zote huwa nawaambia wenzangu kwamba hakuna haja ya
kutukanana wala kupakana matope. Huwa nawaambia tusikwaruzane wala
tusitukanane kwa sababu hakuna ajuaye Mwenyezi Mungu amemuandaa nani
miongoni mwetu,” alisema.