Jumatano, 17 Juni 2015
leo ni patashika nguo kuchanika ni kati ya ilemi fc na stendi fc ni mwaiteleke cup ndani mwenge nusu fainali
yale mashindano ambayo yanayoshika kasi katika mkoa wa mbeya mwaiteleke cup leo yanaendelea kwa kuzikutanisha timu mbili bora kabisa zilizopo mkoani mbeya timu ya stendi fc pamoja na ilemi fc katika uwanja wa shule ya msingi mwenge .nikianza kukupa historia kidogo ya timu zote mbili katika mashindano ambayo yamefanyika katika uwanja wa shule ya msingi mwenge ,timu ya stendi fc aijawahi kuchukua ubingwa katika uwanja wa mwenge.ila timu stendi fc ni timu yenye mipango mingi hasa wanapokuwa uwanjani timu yao ina mashabiki wa kutosha wanashangilia mwanzo mpaka mwisho.ilemi fc wanajiita timu ya taifa wakicheza leo katika uwanja wao wa nyumbani wana kila sababu ya kushinda katika mchezo wa leo kwanza wapo kwao ndio timu inayoongoza kwa mashabiki wengi ni timu ambayo tayari imeshachukua ubingwa mara kadhaa katika mashindano anmbayo yanafanyika katika uwanja wa shule ya msingi mwenge .mkurugenzi wa mashindano ya mwaiteleke cup eliud mwaiteleke anasema uwezekano wa kupata wachezaji bora na wanaojielewa upo kama wadau wa soka watakazia katika kukuza vipaji vya vijana mkoani mbeya.