MASHINDANO YA KAJUNA CUP YAMEFIKIA PATAMU MAJENGO NJE
KAJUNA CUP IMEENDELEA TENA SIKU YA JANA JUMAPILI KATIKA UWANJA WA SHULE YA MSINGI MBATA KWA KUZIKUTANISHA TIMU MBILI BORA MAJENGO FC NA MAVETERANI. WALIKUWA MAVETERANI WA KWANZA KULIONA GOLI LA MAJENGO KATIKA KIPINDI CHA KWANZA HADI KIPINDI CHA PILI KINAANZA MAJENGO WALIKUWA NYUMA DHIDI YA MAVETERANI. DK CHACHE TU ZA KIPINDI CHA PILI KILIPOANZA MAVETERANI WALIJIPATIA GOLI LA PILI BAADA YA MABEKI WA MAJENGO KUJISAHAU KUWAKABA WASHAMBULIAJI WA MAVETERANI.MAJENGO WALIFANIKIWA KUJIPATIA GOLI LA KWANZA .PAMOJA NA GOLI ILO KUFUNGWA MAVETERANI WALIONEKANA MOTO WA KUOTEA MBALI WALIWEZA KUJIPATIA GOLI LA TATU NA LA USHINDI. HATA HIVYO MCHEZO ULIINGIA DOSARI BAADA YA MASHABIKI WA MAJENGO KUMNASA MAKOFI MSHIKA KIBENDELA.NA KUFANYA MCHEZO REFA KUWEZA KUMALIZA KUTOKANA NA VURUGU ZILIZOFANYWA NA TIMU YA MAJENGO FC .