Jumanne, 2 Juni 2015

Dokta Slaa:Chama cha mapinduzi kijiandae kisaikolojia kukabidhi dola kwa amani baada ya uchaguzi mkuu.


Katibu mkuu wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA Dakta Wilbroad Slaa,amekitaka chama cha mapinduzi kijiandae kisaikolojia ili kikabidhi dola kwa amani baada ya uchaguzi mkuu Oktoba mwaka huu,kwa vile chama hicho tawala hakiwezi kuchaguliwa tena na wananchi,kufuatia kuongeza idadi ya maadui watatu waliokuwepo ambao ni ujinga, maradhi na umaskini, na sasa kuwepo maadui wengine wabaya zaidi rushwa na ufisadi wa kutisha, wanaofanya wananchi wakose huduma muhimu.
Akiongea na mamia ya wakazi wa manispaa ya sumbawanga mkoani rukwa,dakta slaa amesema kwa sasa chama cha mapinduzi hakina jambo jipya linaloweza kubadilisha maisha ya watanzania,zaidi ya serikali yake kufanya ufisadi wa kutisha unaoripotiwa kila siku na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali CAG,hali inayowafanya wananchi wakose imani kabisa na kuonyesha hasira zao kwenye sanduku la kura,na ngome zake ikiwa ni pamoja na ya mkoa wa rukwa kuangushwa.
 
Akitoa ufafanuzi juu ya wimbo wa kulitaka jeshi la polisi kutowapiga mabomu kwa vile ni serikali ijayo,amesema mara tu ukawa watakapochukua dola wataishughulikia sheria ya jeshi la polisi, ili kuliondoa jeshi hilo kwenye vitendo vya ukandamizaji, kwa vile ni sheria ya kikoloni.
 
Mapema wakitoa ushuhuda baadhi ya viongozi akiwemo katibu wa mkoa huo ambaye ni diwani wa kata ya kaengesa Bw.Ozem Chapita,wamesema wamebadilisha utendaji kwenye maeneo yao bila ya kuathiri maisha ya wananchi, ikiwa ni pamoja na uchangiaji wa ujenzi wa vyumba vya maabara katika shule za Sekondari.