Jumatano, 8 Aprili 2015
YANGA NUKSI IMESHINDA BAO 8
Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Afrika Yanga SC wameendeleza wimbi lao la ushindi baada ya leo kutoa kichapo kitakatifu kwa Coastal union cha magoli 8-0 katika mchezo wa ligi kuu ya vodacom uliochezwa katika uwanja wa Taifa.
Katika mchezo huo Yanga walifungua ukurasa wao wa magoli katika dakika ya 10 kupitia kwa Hamisi Tambwe, akiunga mpira wa faulo kwa kichwa.
Kabla coastal hawaja kaa sawa walijikuta wakifungwa goli la pili katika dakika ya 24 kupitia kwa Saimon Msuva kabla ya Hamisi Tambwe kufunga goli 3 katika dakika ya 38 na kuipeleka yanga maumziko wakiwa mbele kwa goli 3-0.
Katika kipindi cha kwanza Yanga walionekana kuwa na dhamira ya kuondoka na maogli mengi katika mchezo wa leo na kujikita vizuri katika usukani wa ligi kuu ya vodacom.
Mwanzoni mwa kipindi cha pili Hamisi Tambwe alifunga goli lake la tatu na kupelekea kufunga hatrik yake ya pili katika misimu yake miwili ya ligi kuu ya Tanzania Bara wakatia akiifungia yanga goli la 4 katika dakika ya 46.
Amisi Tambwe katika dakika ya 49 alihusika katika kutengeneza goli kwa Kpah Sherman na kuindikia yanga goli lake la kwanza katika ligi kuu, ikiwa ni goli la tano kwa yanga hii leo.
Katika dakika 15 za mwisho Yanga walifanikiwa kufunga magoli 3 yaliyofungwa na Saimon Msuva, Hamisi Tabwe na Salim Telelea na kupelekea mchezo kumalizika kwa yanga kuibuka na ushindi wa goli 8-0.