Jumamosi, 18 Aprili 2015

SIMBA YAENDELEZA UTEJA KWA MBEYA CITY

IMG_0160
Mabingwa wa kombe la mapinduzi Sima SC wameendelea kupata dhahama kila wanapokutana na Mbeya city baada ya leo kukubali kichapo cha goli 2-0 kutoka kwa wagonga nyundo hao wa Mbeya.

Katika mchezo wa leo wa ligi kuu ya vodacom uliochezwa katika uwanja wa Sokoine mjini Mbeya, Mbeya city walifunga magoli yao katika kila kipindi cha mchezo, ambapo mchezo ulikuwa uko sawa kawa pande zote mbili ndani ya dakika 90.

Mbeya city waliandika goli lao la kwana katika dakika ya 45 kupitia kwa Paul Nonga na kuipeleka Mbeya city mapumziko wakiwa mbele kwa goli 1-0.

Katika dakika ya 66 Mbeya city waliandika goli la pili kuptia kwa Peter Mwalyanzi na kupelekea mchezo kuisha kwa Simba SC kukubali kichapo cha goli 2-0 toka kwa Mbeya city.

Toka Mbeya city ianzishwe wamekutana na Simba SC katika michezo ya ushindani mara nne, ambapo Mbeya city amefanikiwa kushinda michezo mitatu na kutoka sare mchezo mmoja tu.