Alhamisi, 14 Mei 2015

JEMEDARI AULA TFF, MORAD NA NYONI WAPEWA MIKATABA MIPYA AZAM FC


Aliewai kuwa meneja wa Azam FC Jemedari Said amepata ulaji ndani ya TFF ikiwa ni baada ya kuondolewa katika wadhifa wake ndani ya Azam FC , ambapo katika mfumo mpya wa uongozi wa Azam FC hauruhusu kuwepo kwa wadhifa huo ndani ya timu.

Msemaji wa Azam FC Japhari Iddi Maganga amesema kuwa muundo mpa wa uongozi ndani ya Azam FC hauruhusi wadhifa wa meneja wa timu na hivyo kupelekea uongozi wa azam FC kumalizana na Jemedari.

Maganga amesema kuwa shunguhli za menja wa timu zimeambatanishwa na cheo kingine, katika mfumo wa uongozi mpya wa azam FC.

Katika hatua nyingine msemaji wa TFF, Bakari Kizuguto amethibitisha kuajiliwa kwa Jemedari Saidi ndani ya TFF katika kitengo cha ofisa maendeleo kwa soka la vijana.