Alhamisi, 14 Mei 2015

YALIYOJILI USIKU WA KUAMKIA LEO HUKO BURUNDI


Kumekuwa na mapigano usiku kucha katika mji mkuu wa Burundi ambako kulikuwa na jaribio la mapinduzi ya kutaka kumng’oa madarakani rais, Pierre Nkurunziza.
Rais huyo ameshindwa kurejea nchini mwake kutoka katika mkutano wa viongozi wa kanda,baada ya ndege yake kugeuza kurejea ilikotokea.
Ingawa askari watiifu kwa rais huyo wamedai kuzima jaribio hilo la mapinduzi yaliyokuwa yakiongozwa na meja jenerali Godefroid Niyombare dhidi ya rais wao,na kwamba udhibiti wan chi uko mikononi mwao na hasa katika maeneo muhimu ya mji mkuu wan chi hiyo ,Bujumbura.
Makabiliano ya risasi yamesikika karibu na vituo vya redio na runinga .mwandishi aliyeko Burundi amesema kwamba ameshuhudia jeshi likiwa limegawanyika pande mbili ,na haijulikani nani ameshikilia udhibiti wa nchi kwa sasa.
Rais Nkurunziza amekosolewa kwa haja yake ya kuwania muhula wa tatu wa uongozi nchini Burundi ,maamuzi ambayo yalisababisha wiki kadhaa za maandamano ambapo watu ishirini wameripotiwa kupoteza maisha.
Chanzo: BBC