Jumatano, 15 Aprili 2015

Sad: Mcha Khamis Afariki Dunia

 Sad: Mcha Khamis Afariki Dunia
TANZIA!
Khamis Mcha Khamis ‘Viali’ ambaye ni mchezaji wa Azam FC pamoja na timu ya taifa ya zanzibar ‘ Zanzibar Heroes ‘ na ile ya Muungano ‘Taifa Stars ‘, amefiwa na Baba yake mzazi hapo jana.
Mzee Mcha Khamis amefariki baada ya kuugua kwa muda mrefu, alisumbuliwa na matatizo ya njia ya mkojo, taratibu za mazishi zinafanywa.
Klabu Azam FC, Uongozi  wa HARUBUTZ unampa pole Viali na familia yake na kuwataka wawe na subra katika kipindi hiki kigumu. Innalillah wa innaillaih rajiun!