Jumatano, 15 Aprili 2015

RADI YAUA KIGOMA

 Radi Yaua Wanane Kigoma.
NA:DAUD MWALIM
MWANDISHI WA HARUBUTZ
Watu nane wamefariki dunia na wengine 15 kujeruhiwa vibaya baada ya kupigwa na radi ambayo chanzo chake kimeelezwa kuwa ni kunyesha kwa mvua kubwa iliyodumu kwa takribani saa tatu katika Manispaa ya Kigoma Ujiji.
Taarifa za awali zimeeleza kuwa miongoni mwa watu waliofariki ni pamoja na wanafunzi sita, mwalimu mmoja na raia mmoja ambaye ni mkazi wa kijiji cha Bangwe mkoani Kigoma
Shuhuda wa tukio hilo ambaye ni Mwalimu wa darasa la kwanza shuleni hapo, Melina Sililo amesema, wakati alipokuwa akiendelea na kufundisha aliona wingu likitanda na Mvua ikaanza kunyesha jambo lililosadabisha giza.
Amesema hali hiyo ilimfanya ashindwe kufundisha na wakati huohuo radi zilipigwa na moto ukatanda darasa zima ambapo yeye pamoja na watoto zaidi ya kumi walianguka.
Waliopoteza maisha kutokana na tukio hilo ni mkazi wa kijiji cha Bangwe Focus Ntahaba, Mwalimu Eliza Mbwambo, Wanafunzi Yusuph Athman, Hassan Ally, Fatuma Sley, Zamda Seif, Shukran Yohana na Walupe Kapupa.