Jumatano, 15 Aprili 2015

BASI LA AIR JORDAN LAPATA AJALI MTU MMOJA AFARIKI DUNIA



MTU mmoja amefariki Dunia, na wengine ishirini kujeruhiwa kufuatia ajali iliyohusisha basi kampuni ya Air Jordan na gari ndogo  baada ya kuacha njia na kuanguka katika eneo la migua wilaya ya Nzega mkoani Tabora.
HARUBU TZ imezungumza na kamanda wa mkoani humo Suzan Kaganda, amesema kuwa chanzo cha awali cha kutokea kwa ajali hiyo kinaonesha ni mwendo kasi wa basi hilo ambalo lilikuwa likitokea jijini Mwanza kuelekea jijini Dar es salaam.
Kamanda Kaganda ameeleza kuwa hadi sasa maiti imeshatambuliwa na ndugu wa marehemu ambapo majeruhi wote wa ajali wapo katika hospitali ya Nzega mkoani humo.