Beki wa FC Barcelona Gerard Pique Bernabeu ambaye alikuwepo kwenye kikosi cha Hispania usiku wa kuamkia hii leo, amesema hawana budi kusahau yaliyopita na kuganga yajayo.
Pique ambaye ni mwenziwake mwanamuziki Shakira Isabel Mebarak Ripoll, aliinadi kauli yake kupitia mtandao wa Twitter ambapo mashabiki wake wameoinyesha kumuunga mkono.
Beki huyo mwenye umri wa miaka 28, amesisitiza kwamba kufungwa na Uholanzi kunaendelea kuwaonyesha udhaifu uliopo kwenye kikosi chao hivyo hawana namna ya kukubaliana na mtokeo ambayo siku za usoni yatawasaidia.
|