Jumanne, 31 Machi 2015

KUTOKA MJENGONI DODOMA

Serikali Yakiri Kuwepo Kwa Udhaifu Wa Ufuatiliaji Matukio Ya Uhalifu Dhidi Ya Albino

Jumla ya matukio 56 tangu mwaka 2006 juu ya uhalifu dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi yaani Albinism yameripotiwa serikali imebainisha.
Akizungumza mjini Dodoma jana, wakati akijibu maswali yanayohusiana na matukio yanayowakumba watu wenye ulemavu wa ngozi hapa nchini Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Pereirra  Silima alitaja mgawanyiko wa matukio hayo ni pamoja na matukio 41 yakisababisha vifo vya watu 43 , matukio 13 yakisababisha watu 13  kujeruhiwa na mengine mawili yakisababisha watu wawili kupotea.
Aidha akijibu swali la namna gani serikali inavyowajibika katika kuhakikisha watu wanaosababisha matukio hayo wanaashugulikiwa  Silima alisema kuwa bado Serikali inawasaka watu ambao wanatuhumiwa kujihusisha na matukio ya hivi karibuni yaliyowasababishia ulemavu  na vifo vya  watu hao pamoja na kuwatafuta watu 2 wenye ulemavu wa ngozi waliopotea.
Kwa sasa Taifa la Tanzania lipo katika sintofahamu kutokana na matukio yanayoendelea dhidi ya watu wenye ulemavu wa Ngozi -albinism- hali inayowafanya watu wa jamii hiyo waishi maisha ya mashaka.