Jumamosi, 11 Aprili 2015

MBEYA CITY WAAPA KUWATUNGUA YANGA INTERNATIONAL JUMAPILI TAIFA

                                                  
MSHAMBULIAJI wa kutumainiwa  wa Mbeya City Fc, Themi Felix amesema  City itaondoka na ushindi kwenye mchezo wa ligi kuu ya soka Tanzania bara dhidi ya Yanga  unaotarajiwa kuchezwa jumapili kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar Es Salaam.
Themi ameyasema hayo mapema jana mara baada ya kumalizika kwa mazoezi ya asubuhi kwenye uwanja wa Uhuru jijini hapa huku akitupilia mbali dhana ya mashabiki wengi wa soka nchini wanaoamini Yanga itapata matokeo kama iliyopata kwenye mchezo uliopita.
“Watu wengi wanaamini Yanga itashinda kama ilivyoshinda mchezo uliopita, kucheza na City ni tofauti sana na kucheza na timu nyingine hilo nadhani hata wao wanalijua, tumejiandaa vizuri na imani yangu kubwa tutapata ushindi” alisema
Aidha Themi ambaye mpaka sasa tayari amekwisha ‘pachika’ wavuni mabao 4 aliweka wazi kuwa mchezo ambao City ilicheza dhidi ya Azam Fc kwenye uwanja wa Chamanzi ulikuwa mzuri na mkubwa  huku akiapa kuwatungua Yanga jumapili.

                                                      JUMA NYOSSO KULIA

Katika hatua nyingine Mlinzi Juma Nyoso aliyecheza umchezo wake wa kwanza  jumatano iliyopita baada ya kukosekana dimbani takribani miezi miwili kufutia adbabu ya kutokucheza mechi nane amesema Yanga hawana  chao kwenye mchezo wa jumapili.
“Tulicheza vizuri mchezo uliopita, binafsi najiamini na ninaweza kusema Yanga hawana chao jumapili City hii siyo ile waliyoikuta mbeya wajiandae  vizuri vinginevyo wanaweza kutoka vichwa chini baada ya dakika 90 kwenye uwanja wa Taifa kwa sababu tumedhamiria na tunajua tuna pointi tatu hapo” alisema.