Jumamosi, 25 Aprili 2015

KUELEKEA MCHEZO WA LEO MWABUSI ANENA KUHUSU KUWAKOSA WACHEZAJI WAKE WATATU


Kikosi cha Mbeya City Fc leo kinashuka kwenye uwanja wa Sokoine kusaka pionti tatu muhimu mbele ya Kagera Sugar kutoka Bukoba mkoani Kagera  kwenye mchezo wa ligi kuu ya soka Tanzania Bara huku ikiwakosa nyota wake  watatu Steve Mazanda na Yusuph Abdalah walio majeruhi pia  Themi Felix anayetumikia adhabu ya kadi nyekundu.
Akizungumza kuelekea mchezo huo Kocha Mkuu wa City, Juma Mwambusi, amesema licha ya kuwakosa nyota hao   amekiandaa vizuri kikosi chake  kwa lengo la kuibuka na ushindi katika mchezo huo akiwa na hesabu za  kusogea juu kwenye msimamo wa ligi.
“Nimewaandaa vizuri wachezaji wangu, lengo letu ni kushinda  ili tupate pointi tatu ambazo zitatusogeza juu kwenye msimamo, nitawakosa Themi,Mazanda na Sisalo lakini sina shakana hilo, kwa hesabu za haraka najua  mchezo huu utakuwa mgumu kwa sababu  tunaihitaji nafasi ambayo wapinzani wetu wapo na wao bado wanahitaji kubakia walipo  ni wazi mchezo utakuwa  na ushindani mkubwa lakini nina imani tutaibuka washindi” alisema.