Jumamosi, 25 Aprili 2015

KATIBU WA VIJANA TAIFA KUPITIA CCM AWAPA HABARI YAO WENYE NIA YA UBUNGE MBEYA

Katibu mkuu wa vijana taifa kupitia chama cha mapinduzi leo. sixtus mapunda  amewaomba vijana kuwa na umoja wa kujenga chama na kuacha kuwekwa makundi na baadhi ya viongozi   ambao kila mmoja ameonekana akitangaza nia ya kugombea ubunge ndani ya jimbo la mbeya.ameshangazwa na kauli za mh.mbunge wa jimbo la mbeya mjini joseph mbilinyi kutowajenga wana mbeya kuwa wamoja na badala yake amekuwa ni mtu wa kugawa makundi ya kushabikia mabaya .akitolea mfano mtu mwenye njaa ukimjaza hasira  uwa hasira  zinajaa mara mbili amewaasa wana mbeya hasa vijana wajiulize sugu amewapatia elimu gani wapiga kura  wake zaidi ya kuwashawishi wananchi kuandamana na kuchoma barabara moto .amehaidi  kuwa jimbo la mbeya mjini safari hii ni la kwao.pamoja na hayo Mwenyekiti wa vijana mkoa wa mbeya Amani kajuna amewaomba vijana wa ccm kuwa na umoja katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi wa mwaka 2015 wa rais na wabunge pamoja na madiwani .