Huku hali ya amani ikianza kurudi katika baadhi ya mitaa iliyogubigwa
na vurugu za kupinga na raia wa kigeni nchini Afrika Kusini imeelezwa
kuwa raia wa nchi hiyo wanaogopana wenyewe kwa wenyewe.
Baadhi ya raia walipohojiwa na BBC, moja ya ripoti zilizoruka kwenye
kipindi cha Amka na BBC walisema pamoja na hali kutulia lakini kwenye
mizunguuko na shughuli zao za kila siku kila mmoja anamuogopa mwenzake.
“Huwezi kumuamini hata jirani yako”, alisema mmoja wa wahojiwa.
Nchi ya Afriaka kusini ilikumbwa na ghasia zilizosababisha watu
kadhaa kufariki huku raia wapatao mia tatu kukamatwa kwa kusababisha
vurugu kwa raia wakigeni.
Takwimu zinaonyesha Afrika Kusini inaidadi ya wageni wapatao milioni mbili sawa na asilimia nne ya watu wote wa nchi hiyo.
Tangu juzi kumeanza kufanyika maandamano ya amani kupinga vitendo hivyo,
vilivyoitia doa nchi ya Afrika ya Kusini kwa mataifa mengine.