Jumamosi, 25 Aprili 2015

MBEYA CITY YAENDELEZA DOZI KATIKA UWANJA WAKE WA SOKOINE


Mbeya city imefanikiwa kujihakikishia kusalia katika ligi kuu ya Tanzania bara na kukwea mpaka nafasi ya 5 katika msimamo wa ligi kuu ya vodacom baada ya leo kufanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 2-0 mbele ya Kagera sugar.

Mbeya city hii leo walikuwa katika uwanja wake wa nyumbani, uwanja wa Sokoine na kufanikiwa kuibuka na ushindi huo huku kila goli likifungwa katika kila kipindi.

Mbeya city waliandika goli lao la kwanza kwa mkwaju wa penati katika dakika ya 47, ulipigwa na Raphael Alfa, huku goli la pili likifungwa na Deusi Kaseke.