harubutz.blogspot.com
Ni mapokezi ya katibu Mkuu wa CHADEMA Dr Willibrod Slaa akitokeaa
nchini Marekani ambapo alipata mwaliko kutoka kwa Gavana wa Jimbo la
Indianaambapo pia ni meya wa jiji la Indianpolice lilipo katikati kidogo
ya Marekani mwaliko ambao uliambatana na mwaliko kutoka vyuo vikuu
vinne ambao mwaka mmoja na nusu vyuo hivyo vilishawai kutuma mwaliko kwa
chama hiki .
Akielezea ni jinsi gani alivyoweza kutekeleza dhana ya hakuna kulala
kwa vitendo kwani ameweza kutembea umbali mrefu akiwa angani mwendo
takribani wa masaa ishirini na tatu, Huku akielezwa kufarijika na
mapambano yanayoendelea ya kutafuta uongozi pia alieleza kuona picha
nyingi na kupata habari kutoka katika mitandao ya mapambano na kupongeza
zinduzi wa mafunzo ya viongozi na wenyeviti wa serikali ya mitaa
uzinduzi uliofanyika katika uwanja wa sabasaba PTA wiliya ya Temeka
jijini Dar es Salaam.
Huku akisema katika zihara yake wenyeji wake walishangazwa na picha
ambazo zilionyesha vikao vya CHADEMA ambavyo vimeudhuriwa na wanachama
wengi kitu ambacho aliweza kuewaeleza kuwa ni moja ya dhamira ya
watanzania kutaka kufanya mabadiliko na sio mjini tu mpaka vijijini hali
ni hiyohiyo.
Akieleza mambo aliofanya akiwepo katika zihara hivyo Dr Willbrod Slaa
misingi ya zihara ni kwenda kuimarisha mauhusiana mahusiano baina ya
CHADEMA na serikali ya jimbo la Indiana, Akifafanua maana halisi ya
jimbo Dr Slaa amelielezea kuwa jimbo ni kama Nchi ambapo kule huita
STATE.
Huku akiwakumbusha wananchi na wanachama waliojikoze kwenda kumpokea
kuwa dhana ya chadema katika chaguzi zilizopita ilikuwa na sera ya
kuunda majimbo swala ambalo wenzetu ndio wamelitekeza na kuleta
mafanikio makubwa sana katika eneo husika la kila jimbo.akisisistiz
akusema mfumo wa jimbo ni kila jimbo huwa na kiongozi wake na serikali
yake hivyo jambo ambalo kila serikali ya eneo husika hupikagia maslahi
na msukumo wa maendeleo.
Akielezea umuhimu wa mausiano hayo Dr Slaa alisema mahusiano hayo ni
kwasababu anajua chadema inakwenda kushika Nchi na ndio maana chadema
husisitiza mausiano na nchi ambazi zitakwenda kushirikiana nazo ambapo
ikiwa madarakani na kusisitiza kusema Marekani kila jimbo linaweza
kutengeneza mahusiano na nchi yoyote bila kuishikisha serikali kuu.
Akilielezea jimbo la Indiana ambalo miaka thelasini iliyopita ilikuwa
ni maskini na ilikuwa ikijishughulisha na maswala ya kilimo na ufugani
lakini leo hii nchi hiyo imeweza kuwa ni nchi inayosimamia katika
maswala ya viwanda na kilimo na ufugaji wa kisasa. Dr Slaa alisema
alipokuwa Indiana alifanikiwa kutembele shamba la ufugaji lenye ngombe
elfu kumi ambapo kila ngombe mmoja hukamuliwa lita 135 jambo ambalo hata
kwetu Tanzania linawezekana ikiwa serikali itasimamia kikamilifu suala
ya ufugaji na kilimo kicho sahihi kwa kuwawezesha wakulima na wafugaji
huku akishangazwa na upotevu wa malighafu nyingi kupotea zitokanazo na
ufugaji kama vile ngozi, kwato pamoja na pembe.
Akiwaeleza wanachama na wananchi waliojitokeza kumpokea kuwa
Watanzania wamekalia Dhahabu na kueleza anapo zungumzia Dhahabu
hamanishi madini pekee yake ila ni pamoja na uwanja wa ndege pamoja na
bandari, Huku akiufanananisha uwanja wa ndege wa jijini Dar es Salaam
kuwa ni mara kumi ukiuliknganisga na uwanja wa ndege wa Indiana.
Akisisitiza kusema ni aibu kubwa sana kukuta ndege mbili jambao ambalo
ni aibu kwa taifu na inaonyesha dhahiri kuwa nchi imekufa kiuchumi kwani
alipokuwa kaibadilisha ndege akiwa Qatar alipanda ndege yenye uwezo wa
kubeba watu mia mbili lakini ndege hiyo hakuwa ha tan a watu hamsini hii
inaonyesha dhahiri kuwa nchi umeshuka kiuchumi.
Huku alisisitiza kusema CHADEMA haina ugomvi na wawekezaji kwani Nchi
zinazoendelea laziwa ziwe na wawekezaji lakini ugomvi wa CHADEMA ni kwa
wawekezaji mafisadi ambao wanaingia mikataba ya siri na serikali kwa
maswahi yao binafsi, Huku akieleza mafanikio ya Nchi za wenzeku kuwa ni
kuwa hivyo basi tunaitaji mambo muhimu kutoka kwao ili kuweza kuleta
msukumo katika maendeleo ya NChi kama vile technologia, elimu pamoja na
nyenzo hivyo ni vitu ambavyo vinaleta msukumo wa maendeleo katika Nchi.
Akigusia swala la elimu kutoka kwa Nchi za wenzetu Dr Slaa ameeleza
kuwa vyuo vya wenzetu huzalisha wataalamu na kuwatumia tofauti na vyuo
vyetu ambavyo vimekuwa ni sehemu ya kuchukulia vyetu na kuwaacha
wataalamu wetu wakiwa wanazagaa mitaani jamabo ambalo huwezi kulikuta
kwa wenzetu.
Akitolea mfano wa mabadiliko ya vyou ambavyo vilikuwa nu vyuo vya
professional na badala yake kuvifanya kuwa vyou vikuu jambo ambalo
limeshusha utendaji katika jamaa kwani vyuo vikuu huzalisha academic na
professional huzalisha watendaji jambo ambalo wenzetu wamebakisha vyuo
vyao vya professional kubaki kuwa hivyo hivyo na vyuo vikuu kuwa ni vyou
vya kuzalisha academic.
Akijibu swali kutoka kwa mwandishi wa habari swali ambalo alimuliza
Dr Slaa anatoa kauli gani kutokana na serikali kushindwa kukamilisha
mchakato wake wa kura za maoni ya katiba na swala la uwandikishaji kwa
mfumo wa BVR, akijibu swali hilo Dr Slaa ameelza kuwa ameshaliongelea
swala hio na kuwataka serikali hususana Kikwete kumalizia uongozi wake
kwa usalama na kuiacha Nchi kama alivyoikuta asijaribu kuiingiza Nchi
katik machafuko na wala asijaribu kuhairisha uchaguzi kwani ndio swala
kubwa litakalo pelekea Nchi katika machafuko.Akisisistiza kusema katika
zihara yake Nchi Marekani hawatumii BVR na kusema BVR ni ufisana kwani
na kuwakumbusha kwa waliofatilia swala hili tenda ya BVR ilikataliwa na
Mamlaka na ununuzi wa umma na baada yake wakaipitisha kinyemela lengo
kuu ni kutaka kupunguza wapiga kura na ndio maana walianza kuwaandikisha
sehemu ambazo wanaamini kuwa ni ngome ya CCM. Akitoa tamko Dr Slaa la
kusema pamoja na Tume kuwa na mapungufu yake lakini tayari walishakaa na
Kikwete tarehe 31/8/2014 na kukaa tena tarehe 8/9/2014 na kukubaliana
kupunguza mzigo kwa serikali kwa mambo amabyo sio lazima kwa mfano kura
ya maoni sio jambo la lazima sio swala la kikatiba ila ni swala la
kisheria na kumtaka kuelekeza fedha katika serikali za mitaa amabayo ni
maandalizi ya kuawaandikisha wapikagaru ambapo tukielekea uchaguzi mkuu.
Akisisitiza kusema Raisi alipendekeza kwa mdomo wake na kama ni
uwongo atoe kauli ya kudhibitisha kuwa swala hilo ni la uongo ambaye
yeye ndio aliyesema tutaahirisha zoezi la kupiga kura hadi uchaguzu nkuu
ili kuokoa fedha lakini baadae akageuka na kutangaza tarehe jamabo
ambalo halikuwa katika mamlaka yake, sasa tuonaona serikali ilivyotumia
fedha nyingi sana katika kufanya kampeni na kufanya mchakato mzima
katika jamabo hillo ambalo leo hii limeishia njiani.
Akijibu swali la pili kutoka kwa mwandishi wa habari mwingia
aliyeuliza ni nini tamko la chadema au ni maamuzi gani wanataka
kuyachukua juu ya serikali katika utumiaji mbaya wa fedha za umma au ni
kwenda Mahakamani, Kijibu swalli hilo Dr Slaa aliwaeleza kuwa chadema
haina mpango wa kwenda mahakamani kwani kuna kesi nyingi ambazo bado
hazijasikilizwa.
Akijibu swali la nyongeza ambalo limeuliza anatoa kauli gani juu ya mauwaji yanayoendelea south afrika
Dr Slaa alisikitisha na mauuwaji hayo na kuitaka serikali kutolea
tamko nini maana ya ubalozi wa Tanzanio kazi yake uliopo Nchini Afrika
ya kusini na kuinya Tanzania kuwa yanayotokea Afrika ya kusini ni
matokeo ya serikali kushindwa kuwapatia wananchi wake mambo muhimu hivyo
sio ajabu na hapa Tanzania ikatokea machafuko ya aina hiyo.