Alhamisi, 23 Aprili 2015

WASOMI WALAUMIWA KWA KUSHINDWA KUTATUA MATATIZO KWENYE SEKTA YA MADINI



WASOMI nchini wamelaumiwa kwa kushindwa kutumia taaluma zao katika kuyatafutia ufumbuzi matatizo yanayowakabili wananchi kwenye sekta ya madini, licha ya kodi za wananchi kutumika kuwasomeshea.
Akizungumza na kituo hiki Mwanasheria na Mtafiti kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binaadamu -LHRC- Flaviana Charles  amesema licha ya matatizo hayo kutokea kwenye jamii zilizojaa wasomi wa kila kada lakini wameshindwa kuyakemea maovu hayo.
Amesema kuwa tangu kubinafsishwa kwa baadhi ya migodi ya madini nchini, wananchi wanaozunguka maeneo hayo, wamekuwa wakikumbana na kero mbalimbali ikiwemo kunyanyaswa, kucheleweshwa kulipwa kwa mirahada kwenye Halmashauri na wawekezaji hao kushindwa kutoa huduma za kijamii kwa wananchi.