Vinara wa ligi kuu ya vodacom Yanga leo
wanataraji kuwa wenyeji wa Stand United ya Shinyanga katika muendelezo
wa ligi kuu ya vodacom, mchezo utakao chezwa katika uwanja wa Taifa.
Mchezo wa leo ni muhimu kwa yanga kama
wanataka kutangaza ubingwa wa Tanzania bara kabla ya kwenda kuwavaa wa
Tunisia Etoil Du Saheil katika mchezo wa marejeano utakao fanyika nchini
Tunisia.
Nayo stand unite inayokabiliwa na
michezo miwili migumu katika juma hili, watakuwa wanahitaji pointi tatu
kujinusuru kutoshuka daraja, kutokana na kuwa na pointi 38 ambazo
zinawezwa kufikiwa na Polisi Morogoro mwenye pointi 24 akiwa katika
nafasi ya pili kutoka mwisho na Tanzania Prisons aliye katika nafasi ya
mwisho, akiwa na pointi 22.
Katika mchezo wa leo huenda tukashuhudia
urejeo wa Mbrazili Andrew Countinho aliyekosekana kwa majuma 10
kutokana na majeraha aliyokuwa nayo, sambamba na kiungo anae tamba kwa
sasa Salum Telela, aliyekosa mchezo dhidi ya Etoil Du Saheil kutokana na
majeraha.
Endapo Stand unied wakifanikiwa kuondoka
na pointi hii leo katika uwanja wa Taifa, kutapeleka matumaini
Chamanzi, makao makuu ya Azam FC, ambao wanahamu ya kuwa timu ya pili nje ya Simba na yanga kutetea ubingwa wa ligi kuu ya vodacom.
Mkuu wa kitengo cha habari wa yanga
Jerry Muro akizungumza na moja ya kituo cha redio hapo jana alijinasibu
timu yake ya yanga itaibuka na ushindi wa goli 10 hi leo.
Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza yanga walifanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 3-0 katika uwanja wa CCM Kambarage.
Na hii inakuwa ni kwa mara ya pili Stand
united kucheza mchezo wa ligi kuu katika uwanja wa Taifa ambapo mchezo
wake wa kwanza walifanikiwa kutoka sare ya kufungana goli 1-1 dhidi ya
Simba SC.
Kocha wa Stand united alijinasibu
kufanya vyema katika mchezo wa leo hapo jana pale alipokuwa akihojiwa na
moja ya redio nchini, hku akiwategemea zaidi Chanongo na Mnigeria
katika kupeleka zaama katika mitaa ya jangwani hii leo.