membe pia amempa sifa mark mwandosya kwa kusema ni mtu muadilifu ,sio mla rushwa amewambia watu wa mbeya kuwa kama atashindwa kupata nafasi basi yeye atamfanyia kampeni mark mwandosya na kufanya watu wa mbeya kumshangilia kwa vifijo na vigelegele pia amezungumzia mikakati ya kuwawezesha wafanyabiashara wadogo wadogo wakiwemo mama lishe ,bodaboda kuanzisha vikundi vyao na kuanzisha saccos na kuweza kuwasaidia kukopeshana kwa riba nafuu kabisa na kwa muda muafaka .baadae alipata nafasi ya kukutana na wana vyuo mbalimbali na kuzungumza nao katika hotel ya hill view
Alhamisi, 11 Juni 2015
WAZIRI MEMBE ATIKISA MBEYA
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe jana amepata wadhamini zaidi ya 800 .membe amesema akipata nafasi ya kuteuliwa kuwa mgombea wa urais na hatimaye kuwa rais ,amewahidi wakazi wa mkoa wa mbeya kuwaongezea kipato kupitia uwanja wa ndege wa kimataifa wa songwe .akielezea maua ,mboga mboga na matunda ,amewashauri wakazi wa mkoa wa mbeya kujenga majengo makubwa ya kuhifadhi maua na mboga mboga.hata hivyo amezungumzia kuhusu uuzwaji wa mikungu Afrika kusini mkungu wa ndizi ni 15000 wakati mkungu mkoani mbeya mkungu wa ndizi ni 3000 hata hivyo amesema akipata nafasi atawekeza majengo ya usindikaji ili wakulima waweze kuhifadhi vyakula vyao .