Alhamisi, 30 Aprili 2015
WANASIASA WATAKIWA KUACHA KUJIINGIZA KWENYE SHUGHULI ZA KIJAMII KWA LENGO LA KUPATA KURA
CHAMA cha Alliance For Democratic Change-ADC, kimewataka wanasiasa nchini kuacha tabia ya kujiingiza katika shughuli mbalimbali za kijamii kwa lengo la kujitengenezea mazingira ya kupata kura katika chaguzi zijazo.
Akizungumza na blog hii kuhusiana na hali ya kisiasa ilivyo Mwenyekiti wa ADC, SAIDI MIRAJI amesema kuwa kumekuwa na Tabia ya baadhi ya wanasiasa wanaotarajia kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kuanza kampeni za chinichini za kujiingiza katika masuala mbalimbali ya kijamii kama michezo ujenzi wa barabara za mitaa ili kujitengenezea mazingira ya kupigiwa kura.
MIRAJI amewataka wanasiasa wenye tabia hizo kuacha kwani wanapaswa kutambua kuwa uongozi ni wito hivyo waache kuwaona watanzania kama watu wasiojielewa.