Waganda
leo wanapiga kura katika uchaguzi wa rais na bunge, unaofanyika huku
kukiwa na malalamiko ya masanduku ya kupigia kura kufikakwa kuchelewa
katika baadhi ya vituo vya kupigia kura na kufungwa kwa mitandao ya
kijamii.
Leo
asubuhi asubuhi misururu mirefu ya watu ilionekana katika vituo vya
kupigia kura mjini Kampala ambapo zoezi la kupiga kura lilianza kwa
kuchelewa kwa zaidi ya saa moja na nusu kufuatia maafisa wa uchaguzi
kuendelea na matayarisho ya vifaa vya kupigia kura.
Zoezi
hilo la upigaji kura linatazamiwa kukamilika saa kumi jioni saa .Bado
hapajakuwa na taarifa zozote iwapo zoezi hilo litarefushwa kufuatia
baadhi ya vituo kuanza shughuli hiyo kwa kuchelewa.
Mawasiliano ya yamitandao ya jamii yafungwa
Huku
hayo yakiarifiwa mdhibiti wa mawasiliano wa serikali ametangaza
kufungwa kwa mitandao ya kijamii ya Facebook na Twitter na kufunga
mifumo ya kutuma pesa kupitia njia ya simu.
Kwa
majibu wa mkuu wa kamisheni ya mawasiliano nchini Uganda Godfrey
Mutabaazi aliyezungumza na kituo cha radio cha CBS, hatua hiyo
imechukuliwa kwa sababu za kiusalama.
Msemaji
wa wizara ya nje ya Marekani Mark Toner amesema Washington ina wasiwasi
kuwa vikwazo hivyo vya mawasiliano huenda vikasababisha mivutano zaidi
katika nchi ambayo tayari inakumbwa na joto kali la uchaguzi.
Kwa
upande mwingine wanaharakati wa haki za binaadamu wameelezea wasiwasi
wao pia juu ya madai ya kuundwa kwa makundi ya vijana wenye silaha
wanaohusishwa na vyama pamoja na wanasiasa mbali mbali kwa ajili ya
kulinda maslahi ya vyama vyao kwenye uchaguzi huu.
Museveni
aliye na miaka 71 aliyechukua madaraka kwa mara ya kwanza nchini Uganda
mwaka wa 1986 na aliyeshinda uchaguzi mara nne kuanzia mwaka wa 1996,
anakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa wagombea wawili kati ya
wagombea saba waliopo katika kinyang'anyiro cha urais.
Kizza Besigye, aliye na miaka 59, aliyekuwa daktari wa Museveni ndiye mgombea wa kwanza anayempa tumbo joto Museveni.
Besigye
ameshashindwa mara tatu katika safari yake ya kuwania urais nchini
Uganda. Mwingine anayeonekana kutoa ushindani mkali ni Waziri Mkuu wa
zamani Amama Mbabazi aliye na miaka 67.