Hali
ya sintofahamu imeendelea ndani ya bunge baada ya wabunge wote wa
Upinzani kutoka ndani ya bunge mara baada ya Wabunge kuanza kuchangia
hotuba ya Rais.
Baada
ya kipindi cha Maswali na Majibu, yalifuata matangazo na baada ya
Matangazo, wabunge wakaanza kuchangia hotuba ya Rais Magufuli .
Wakati hayo yakiendelea, wabunge kadhaa wa UKAWA akiwemo mbunge wa Ubungo(chadema), Saed Kubenea walikuwa wakiomba muongo wa Naibu Spika ili waongee lakini hawakupewa nafasi.
Naibu Spika alikataa miongozo hiyo na kulitaka Bunge lijikite katika kujadili Hotuba ya Rais. Hali hiyo iliwakera wabunge wa upinzani kwa madai kuwa wamezibwa midomo na hivyo wakaamua kutoka nje ya ukumbi wa bunge

==>Wabunge wa CCM wanaendelea kujadili Hotuba ya Rais.