Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemtumia
salam za pongezi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.
Nape Nnauye kufuatia mchezaji wa Timu ya Taifa ya mpira wa miguu Mbwana
Ally Samatta kutwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika kwa wachezaji
wanaocheza Barani Afrika; iliyotolewa katika mji wa Abuja nchini Nigeria
jana usiku..
Mhe.
Rais Magufuli amemtaka Waziri Nape Nnauye amfikishie salam zake za
pongezi kwa mchezaji huyo ambaye pia ni mchezaji wa kulipwa wa TP
Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Amesema
tuzo hiyo imemjengea heshima na kuleta sifa kwa Mbwana Samatta
mwenyewe, wanasoka hapa nchini na Tanzania kwa ujumla katika medali ya
Soka Kimataifa.
Aidha,
Rais Magufuli amewasihi wachezaji wa soka wote na wadau wa mchezo huo
kuongeza juhudi za kuundeleza mchezo huo ili upige hatua zaidi za
kimaendeleo.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es Salaam
08 Januari, 2016
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es Salaam
08 Januari, 2016