Jumatatu, 17 Agosti 2015

YANGA YASHINDA KWA MBINDE DHIDI YA MBEYA CITY

Yanga imeifunga Mbeya City kwa kuichapa kwa mabao 3-2 katika mechi ya kirafiki iliyopigwa jana kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.

Yanga ambayo imepiga kambi Tukuyu ilipata upinzani mkali kutoka kwa  Mbeya City iliyokuwa nyumbani.
Mabao ya Yanga yalitupiwa kambani na wageni tu, alianza Andre Coutinho raia wa Brazil.
Baada ya hapo, Amissi Tambwe akatupia la pili kabla ya Donald Ngoma raia wa Zimbabwe kupiga la tatu.
Mabao ya Mbeya City yalifungwa na Bakari Slang na Joseph Mahundi aliyefunga katika dakika ya 90.