Michael Mbuzax alisema Endapo atapata nafasi kitu cha kwanza ni kufufua Viwanda vilivyo kufa
Eliudy Mwaiteleke yeye alisema anajua kuwa kuna matatizo mengi ikiwemo masoko kwenye baadhi ya kata Madaraja na Barabara ambazo hata hivyo akutaka kuitolea Ahadi .pia alimshukuru Diwani aliyepita bila kupingwa Mh diwani Duru kwa kuweza kutengeneza baadhi ya Miundo mbinu.
Mgombea mwingine ni Shadrack Makombe ambaye yeye alielekeza nguvu zake kwa kusema ataendeleza ajira kwa vijana ikiwemo tayari ametoa Ajira kwa kufungua kituo cha Matangazo Generation Fm ambacho kimetoa Ajira kwa vijana wa mbeya .
Mgombea Mwingine Nwaka Mwakisu alisema yeye ameanzisha benki ya vijana ambayo tayari imekwisha toa Bodaboda 200 kwa Vijana wa mbeya kwa hiyo anaomba nafasi ili aweze kuendeleza mambo mengine ya kimaendeleo ndani ya jiji la mbeya.
Sambwee Shitambala alisema awezi kuahidi kitu chochote zaidi ya kuitekeleza Ilani ya chama chake amewaomba Wakazi wa mbeya wajitambue Mwakilishi wao atoke miongoni mwao na sio sehemu nyingine na wataheshimika kuwa wamepitisha mtu wa mkoa wao.
Aman Kajuna alisema jiji la mbeya bado vijana ajira ni tatizo zaidi ya vijana wana tatizo la ajira elfu hamsini tatu tu ambao wameajiliwa na kulipwa stahiki zao.Huku kati ya vijana laki moja na elfu tisini hawana Ajira kwa hiyo amewaomba Wakazi wa mbeya kumpa kura.
James Mwampondele alizungumzia amefanya mengi katika jamii ikiwemo kuweka magoli ya netball kwa kina mama na pia kusaidia ujenzi wa uwanja wa sokoine ya kuweka magoli na nyasi,lakini pia amesema endapo atachaguliwa na chama chake atahakikisha anasimamia vizuri ujenzi wa maendeleo ya jimbo la mbeya mjini kwa sababu yeye ni moja ya watu wanaoaminika katika ujenzi wa taifa.
Hosia Mbembela yeye alisema kwanza ni kusimamia Ilani ya chama, pili ni kuwa jirani na wananchi wa jimbo lake.
Samwel Mwaisumbe alinena kwanza ni kulikomboa jimbo la mbeya mjini kutoka kwa wapinzani lakini pia alisema endapo atachaguliwa na chama chake ni kuhutumia mfuko wa jimbo kukopesha wakina mama na vijana ili kuweza kuondokana na tatizo la umaskini.
Naye Mchungaji Jackson Numbi aliwaomba wakazi wa mbeya wampe nafasi ya kumchagua kuwa Mteule wa Chama chake ili aweze kushirikiana na wawekezaji kuwaletea viwanda vya biskuti na juisi,kuondokana na matatizo ya ajira kwa vijana.
Fatuma kassenga yeye alisema ni mzoefu wa siku nyingi kuhusiana na maswala ya siasa Mwaka 2010 aligombea lakini akupata nafasi kutokana na kura kutoweza kutosha amewaomba hasa wa kina mama kumuunga mkono ili aweze kupata nafasi ya kuwa mgombea Ubunge kupitia chama chake cha mapinduzi (CCM).