Diwani wa kata ya luhanga mh.Dira Funika amesema kata ya luhanga inachangamoto nyingi ikiwemo,elimu,miundo mbinu,matatizo ya migogoro ya ardhi .mh.funika amesema ili mambo yaweze kwenda kwa wakati ni lazima awashilikishe wananchi kwa ujumla kuweza kwenda mbele na mikakati yake kwa kufanya vikao na wananchi wake watoe maoni na yeye ayapeleke katika vikao vya baraza la madiwani .alipoulizwa na mtandao huu kuhusu michango ya vyakula katika kata yake amesema utaratibu huo bado aujaanza mh.funika amesema ili kwenda na kasi ya mgufuli ni lazima viongozi wawajibike maeneo yao ya kazi kuwa waaminifu na waadilifu.amewaasa viongozi na watendaji wa kata yake kuwacha kufanya kazi kwa mazoea.mtandao huu umebaini kuwa viongozi wengi hasa katika wilaya ya mbalari wamekuwa wapigaji katika maswala mazima ya ardhi.