Mwenyekiti wa kikao cha Bunge ambaye pia ni Mbunge wa Bariadi Magharibi Andrew Chenge maarufu kwa jina la Mtemi amewataka wabunge kujifunza kwa umakini namna bora ya kutumia kanuni za Bunge.
Mwenyekiti
Chenge amefanya hivyo mara kadhaa alipokuwa akijibu miongozo ya wabunge
kutoka vyama vya upinzani wakiwamo Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea
(CHADEMA), Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe (ACT) pamoja na Mbunge wa
Singida Magharibi Tundu Lissu (CHADEMA).
Kwa upande wa kubenea aliomba muongozo kuhusu mbwa walioingizwa Bungeni, askari polisi kuwavua nguo za ndani wabunge wa kike pamoja na shanga na Hereni zao jambo ambalo haliruhusiwi ambapo Mwenyekiti wa Bunge alimtaka mbunge huyo kutafuta kanuni nyingine ya kupeleka ombi lake kama anadhani hoja yake ni ya msingi.
Kwa upande wa Lissu pamoja na Zitto wenyewe waliomba
miongozo kuhusu mpango wa serikali wa miaka mitano uliowasilishwa na
serikali kupitia wizara ya fedha,kwamba umekiuka kanuni za bunge,ambapo
mwenyekiti aliwajibu kwamba mpango haujakiuka na si mara ya kwanza kufanya hivyo na akaahidi kutoa majibu baadae.
Aidha Mwenyekiti huyo wa Bunge alitoa
rai kwa wabunge wote kuzisoma kanuni za bunge na kuzielewa na mipaka
yake katika namna bora ya kuendesha vikao hivyo vya Bunge.
Hata
hivyo Kikao cha bunge kimeendelea kama kawaida na shughuli zake huku
wabunge wa kambi rasmi ya upinzani wakirejea baada ya kugoma kushiriki
katika mjadala wa kuijadili hotuba ya Rais kwa kigezo cha shirika la
utangazaji la Taifa kutorusha matangazo ya moja kwa moja kuhusiana na
mijadala hiyo.