Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Jamal Malinzi anashiriki katika kongamano la Fainali za Dunia kwa Wanawake zinazofanyika Vancouver- Canada kwa siku tatu kuanzia tarehe 3 - 5 Julai mwaka huu.
Katika kongamano hilo Malinzi ameambatana na katibu mkuu wa Chama cha Soka la Wanawake Tanzania (TWFA), Amina Karuma.
Kongamano hilo la soka la Wanawake linahudhuriwa na nchi 209 wanachama wa FIFA, ambapo hufanyika kila baada ya miaka minne, pindi zinapofanyika fainali za Dunia kwa wanawake.
Miongoni mwa wachangiaji wa kongamano hilo ni mjumbe wa kamati ya Utendaji ya FIFA, ambaye pia aliwahi kuwa Rais wa chama cha soka cha nchini Burundi, Lydia Nskera.