Jumapili, 5 Julai 2015

Ndio ni Chile mabingwa wa Copa America 2015


Sanchez akiwa ameinua Kombe akishangilia na wenzake usiku huu



naam. Usemi huo umedhihirika usiku huu baada ya wenyeji Chile kutwaa ubingwa wa Kombe la Mataifa ya Amerika Kusini, maarufu kama Copa America kwa ushindi wa penalti 4-1 dhidi ya Argentina Uwanja wa Taifa mjini Santiago.
Baada ya sare ya 0-0 ndani ya dakika 120, mshambuliaji wa Arsenal ya England, Alexis Sanchez alifunga penalti ya nne ya Chile na kumaliza mchezo, baada ya Gonzalo Higuain na Ever Banega kukosa mfululizo mikwaj yao. 
Waliofunga penalti za Chile mbali na Sanchez wengine ni Charles Aranguiz, Arturo Vidal na Matias Fernandez, wakati Lionel Messi alifunga penalti pekee ya Argentina. 
Kwa hisani ya bin zubeir