Alhamisi, 30 Julai 2015

MMOJA YA WAGOMBEA UBUNGE ATENGENEZA KUNDI LINALOPITA KWA WANACHAMA KUTOA PESA NA KUSEMA WASICHAGUE MNYAKYUSA AU MSAFA KWANI WAO HAWAPATANI SASA KAZI IPO KWA CCM KUCHUKUA JIMBO KWA MICHEZO HIYO MICHAFU

 Baadhi ya makundi yanayoeneza Siasa chafu ya Ukabila yakiwa yanabadilishana mawazo na mmoja wa Kiongozi wa  Vijana kupitia Uvccm.


Vinara ambao wanasambaza uongo na uchanganishi wa kumpigia kampeni mmoja wa Wagombea ubunge  na kusambaza kuwa Mnyakyusa na Msafa  hawapatani na kuwambia wanachama wamchague huyo mgombea ubunge ambaye yeye si kabila la Mbeya.
Wanachama Wengine ni waliosimama juu ya gari la matangazo ambalo linatembea kwenye kampeni ya kuomba kura hawa nao kazi yao kubwa ni kusambaza fitina za ukabila kuwa Mnyakyusa na Msafa hawafai kuwapigia kura kwani hawapatani.

Katika hali ya kushangaza zikiwa zimebaki siku moja kabla ya kufanyika Uchaguzi wa Wagombea Ubunge na Madiwani ,Leo Katibu wa Wazazi wilaya ya Mbeya Mjini (UWT)Nusura achapwe na mmoja wa wgombea Ubunge baada ya kupeleka shutuma kwa mbunge huyo kuwa Mnyakyusa na Msafa hawapatani ndipo kasheshe ilo lilipoanza na kuamliwa na baadhi ya Wagombea Ubunge kwa matokeo haya ambayo yameanza kujitokeza inaonesha kuna kasumba kubwa ya kutaka kuzidiana katika kugombea kupata kura za kumpitisha Mgombea mmoja ili aweze kupitishwa  kuwa Mgombea Ubunge kwa tiketi chama cha mapinduzi.  hali hii tayari inaonesha uaminifu  kwa viongozi wa ccm kuwa mdogo.Hata hivyo michezo michafu ya kugawa pesa kuanzia 50,000 hadi 30,000 kwenye vijiwe vya bodaboda  na waosha magari imebainika katika kipindi hiki cha kuomba kura .Wanachama mbalimbali kupewa ongo kuanzia 5,000 ,10,000 hadi 20,000 hii imeonekana ni jambo la kawaida na kuwafanya baadhi ya vijana kutafuta ridhiki kupitia wagombea ubunge hao. tutakutajia ni wakina nani ambao wanahusika na michezo michafu hiyo. ITAENDELEA....................................