Mwenyekiti wa Chadema Mbeya mjini John Mwambingija leo alikuwa akiongea na wakazi wa mbata na alisema wakazi wa mbata waache kujipendekeza kwa chama cha mapinduzi (CCM) alisema viwanda vya mbeya vimekuwa ni maghala baada ya kutupwa na Serikali ya chama cha mapinduzi amewaomba wakazi wa mbata kufanya mabadiliko hasa vijana .Alikwenda mbali zaidi kwa kusema Mh mbunge Joseph Mbilinyi amefanya mambo mengi katika kipindi cha miaka mitano ikiwamo kutoa Computer, Nyumba ya walimu iliyopo Nzoho pamoja na kutengeneza Barabara ya nzoho pia alisema kupitia kwa mbunge Sugu amepeleka umeme eneo la Mwansekwa pia aliawaambia jeshi la polisi wajiongeze kwani nchi sasa inabaki mikononi mwa Ukawa.Pia aliwaomba vijana waanze mabadiliko kwani wazee kipindi chao kimekwisha.