Mamlaka
ya chakula na dawa nchini Tanzania TFDA imebaini kuwepo kwa kiwanda
bubu kinachozalisha bidhaa za vipodozi nchini Tanzania zenye lebo ya
SAME inayoonesha kutengenezwa nchini Uturuki kinyume na sheria na
taratibu za kuanzisha kiwanda na bila kukaguliwa na mamlaka hiyo kama ni
salama kwa matumizi ya binaadamu.
Akiongea
hii leo mkurugenzi wa TFDA Hiti Silo amesema kuwa awali walikamata
shehena ya chupa 5,350 za pafyumu zenye thamani ya shilingi milioni 107
na walipomuuliza mmiliki wa duka hilo Dr Mohamed Gwao akasema bidhaa
hizo zimeagizwa toka nchini Uturuki lakini walipofuatilia wakagundua
zinazalishwa hapa nchini maeneo ya Mbagala Tuangoma
Aidha
mamlaka hiyo ilipotembelea eneo hilo ilibaini mitambo mikubwa ya
kuzalisha pafyumu hizo na kuchukua vifaa vyote kwa ajili ya kuvifanyia
uchunguzi zaidi na watuhumiwa wamefikishwa kituo cha polisi.
Mamlaka
ya chakula na dawa nchini inawatahadharisha watumiaji wote wa pafyumu
hizo kuacha kutumia mara moja kwani bidhaa hizo hazijasajiliwa na TFDA
na hivyo ubora na usalama wake haufahamiki.