Mashindano ya mwaiteleke cup Mkoani mbeya yamefika patamu siku ya jumatano patakuwa patashika nguo kuchanika.nusu fainali ya kwanza kati ya Stendi fc wazee wa ng'ata ng'ata wakicheza na watoto wa Ilemi fc a.k.a timu ya taifa.
hata hivyo harubutz imeongea na Mkurugenzi wa mashindano Eliud mwaiteleke ambaye amesema Lengo la mashindano ya mwaiteleke cup ni kutengeneza timu ya kombaini na baadaye kuipa jina la Mbeya united hata hivyo alikwenda mbali zaidi na kuelezea mashindano hayo yamewafanya vijana kuwa pamoja na kuacha vitendo vibaya kama kuvuta bangi,madawa ya kulevya nk.na Tamati ya mashindano ya mwaiteleke cup itakuwa ni tarehe 20 ya mwezi huu .na kutakuwa na mashindano ya kuvuta kamba,kukimbiza kuku,pamoja na zawadi mbalimbali pamoja na hayo amewaomba wananchi kujitokeza kwa wingi siku ya fainali ambazo zitakwenda sambamba na kuchangia damu salama ndugu zetu waliopo hospitalini.pia ametoa maoni yake kuhusu timu ya Taifa stars .ili timu ya taifa ifanye vizuri ni lazima ifanyike mikakati ya kupata vipaji vya vijana chipukizi na ikiwezekana watumie makocha wazawa kama boniface mkwasa,juma mwambusi,abdallah kibadeni nk.alikwenda mbali na kusema inawezekana kwa timu ya taifa kufanya vizuri .pia mwisho alisema analishukuru jeshi la polisi kwa kutoa ulinzi katika mashindano yake ya mwaiteleke cup.