Jumatano, 6 Mei 2015

WAZAZI WATAKIWA KUWALEA WATOTO KATIKA MAADILI MEMA KUEPUKA WIMBI LA WATOTO WA MITAANI



WITO umetolewa kwa Wazazi na Walezi nchini kuwa makini katika kuwalea watoto katika maadili mema ili kuepukana na Wimbi la watoto wa Mitaani.
Hayo yameelezwa na Katibu Mtendaji wa Chama cha Kulea watoto Yatima –CHAKUWAMA, HASANI HAMISI.
Katibu HASSANI ameeleza kuwa jamii ina wajibu wa kusimamia Haki ya mtoto tangu akiwa mdogo na kumuwekea Misingi bora ikiwemo suala la Elimu na Malezi ii kuepukana na Vizazi visivyojua Kusoma na Kuandika nchini.