Jumanne, 5 Mei 2015

OFISA Mtetezi na ushawishi kutoka Shirika linaloshughulika na watu wenye Albinism la Under The Same Sun –UTSS, KONDO SEIF, ameitaka jamii kuungana kupiga vita Imani Potofu.


OFISA Mtetezi na ushawishi kutoka Shirika linaloshughulika na watu wenye Albinism la Under The Same Sun –UTSS, KONDO SEIF, ameitaka jamii kuungana kupiga vita Imani Potofu zinazosababisha Mauaji kwa watu wenye Albinism.Kauli hiyo ameitoa katika Semina ya Siku ya Elimu kwa Radio za Jamii nchini juu ya kuandaa Vipindi vyenye Ujumbe Sahihi ya masuala yanayohusu watu wenye Albinism iliyofanyika katika Kituo cha Radio Jamii Sengerema mkoani Mwanza.KONDO amesema katika jamii kumekuwa na Imani Potofu ambapo Albinism wamekuwa wakiitwa majina yanayolenga kunyanyapaliwa na kusababisha kushamiri kwa vitendo vya Ukatili na mauaji dhidi yao.