Ijumaa, 8 Mei 2015
WATU 8 WAMEFARIKI DUNIA HUKU MAMIA WAKIKOSA MAKAZI KUFUATIA MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA DAR
WATU nane wamefariki dunia na mamia kukosa makazi kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika jiji la Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Said Meck Sadiq amesem vifo hivyo vimetokea jana kufuatia vua kubwa iliyonyesha katika jiji hilo nakusababish mafuriko kuhu baadi ya wananchi wakikosa makazi.
Hata hivyo Mkuu huyo wa Mkoa amesema wananchi waishio mabondeni wamekuwa wakikaidi kuhama katika maeneo hayo licha ya Serikali kuwapatia viwanja. Amesema msaada utakaotolewa na Serikali hautahusisha kuwapatia huduma za matibabu pindi itakapobaini kuwepo kwa baadhi ya wananchi waliopata majeraha kufuatia mafuriko hayo