Jumanne, 12 Mei 2015
SSERUNKUMA NA OWINO KWAHERI SIMBA SC
Klabu ya Simba imeamua kuvunja mikataba na wachezaji wake wawili Raia wa Uganda mlinzi Joseph Owino na mshambuliaji Danny Sserunkuma kwa makubaliano ambayo yameridhiwa na pande zote mbili.
Katika ukurasa wake wa Facebook Owino aliwashukuru mashabiki wa Simba na kuitakia Simba kila la Heri na akatanabaisha kuwa ameamua kuihama klabu hiyo.
Danny Sserunkuma ambaye ni mwezi wa sita tu tangu alipojiunga na Simba naye alifunguka katika ukurasa wake wa Twitter akisema amefikia makubaliano na uongozi wa Simba kuhusu kuuvunja mkataba wake hivyo yeye si mchezaji tena wa Wekundu hao wa Msimbazi.
Simba imemaliza ligi ikiwa katika nafasi ya tatu nyuma ya mabingwa Yanga na Azam waliokamata nafasi ya pili huku nafasi ya Owino ikipotezwa na uwepo wa mzawa Hassan Isihaka wakati Dany Sserunkuma ameonekana si lolote kwa safu ya ushambuliaji ya Simba na nafasi hiyo mara nyingi amekua akicheza Chipukizi Ibrahim Ajib ambaye amepandishwa toka Simba B na kupata mafunzo ya kutosha alipokua Mwadui FC kwa mkopo.