Mnamo 13 mwezi May jenerali
mmoja wa jeshi alitangaza katika redio ya taifa kwamba rais wa Burundi
amepinduliwa na kwamba serikali ya mpito itabuniwa.Lakini msemaji wa
rais alikana habari hizo akidai kuwa kulikuwa na usaidizi mdogo katika
jeshi kwa mapinduzi kutendeka.
Rais wa Burundi Pierre
Nkurunziza ameonya kuwa atalipiza kisasi dhidi ya mtu yeyote ambaye
atashambulia Burundi.''katika taarifa yake amesema kuwa ''hatutakubali
mtu yeyote kuwasha moto Burundi''.
Rais
wa Burundi Pierre Nkurunziza ametuma ujumbe katika mtandao wake wa
tweetter kwa lugha ya kirundi akisema kuwa ''Nilifurahi kuona vile raia
wa Burundi walivyonipokea katika mji wa Bujumbura pamoja na mikoa
mingine
Kuna mazingira ya hofu na
switofahamu katika mji wa Bujumbura kufuatia kufeli kwa jaribo la
mapinduzi kulingana na mkaazi mmoja wa mji huo.Serge Ntabikiyoboka
anasema kuwa hadhani kwamba taifa hilo literejea katika hali yake ya
kawaida hivi karibuni.
Tume ya haki za binaadamu
katika umoja wa mataifa imeonya kuhusu ulipizaji kisasi kufuatia jaribio
la mapinduzi nchini Burundi.Msemaji wake Rupert Coleville amesema kuwa
tume hiyo ina wasiwasi kuhusu matukio ya taifa hilo katika kipindi cha
siku mbili zilizopita.