Jumatano, 6 Mei 2015
KUELEKEA MCHEZO WA YANGA NA AZAM LEO MAJIGAMBO KIBAO
Mabingwa wa tanzania bara Yanga SC leo watakuwa na kazi mbili tu moja ni kukabidhiwa kombe na pili ni kupata pointi tatu muhimu katika mchezo wa leo .katika kuelekea mchezo wa leo Meneja wa timu ya Azam FC Jemedali said amesema wao awana undugu wowote na simba kuwa wao wapo kama walivyo siku zote hivyo kauli za simba za kusema leo watavaa jezi za Azam hizo ni kejeli tu kwani wanajua simba wanataka nafasi ya pili.Kwa upande wa Yanga Mkurugenzi wa mawasiliano Jerry Muro amewaomba wapenzi wa simba wavae jezi za Yanga kwa wingi na kuishangilia timu yake ili waweze kuwabeba katika mchezo wa leo ,Maneno hayo yamepingwa vikali na viongozi wa simba huku wakisema wao hawana nia na nafasi ya pili kwa sasa wanajipanga na msimu ujao wa ligi.