Jumatano, 6 Mei 2015

AZAM FC NA YANGA SC KUPANDA NDEGE TENA SIMBA CHALIIIIIIIIII


Ni mara ya nne mfululizo Azam FC inajihakikishia nafasi ya kuiwakilisha Tanzania katika michuano ya CAF, baada ya leo kufanikiwa kuwafunga mabingwa wa Tanzania bara yanga, na kuipelekea Simba SC kukosa michuano ya kimataifa kwa mara ya tatu mfululizo.

Katika mchezo wa leo uliochezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, ulitawaliwa kwa mvua kubwa, huku kukipelekea mchezo kupoteza mvuto.

Yanga walikuwa wa mwanzo kupata goli katika dakika ya 11 kupitia kwa Andrey Countinho kwa mpira wa adhabu uliopigwa nje kidogo ya eneo la hatari.

Dakika moja baadae Azam FC walisawazisha goli hilo kupitia kwa Bryson Raphael akimalizia pasi nzuri ya Frank Domayo ikiwa ni baada ya Gaudence Mwaikimba kushindwa kufunga goli, kabla ya mpira kumfikia Domayo.

Magoli hayo mawili yalidumu kwa kipindi cha kwanza na dakika 25 za kipndi cha pili, pale mashabiki wa yanga na Azam FC kunyanyuka kwa shangwe kufuatia goli la Aggrey Morice, likiwa ni goli la pili kwa Azam FC katika mchezo wa leo.

Hadi kipenga cha mwisho kinapulizwa Azam FC walikuwa mbele kwa goli 2-1, na kufikisha pointi 48 ambazo Simba SC hawataweza kifikisha.