JESHI la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania –JWTZ- limevitaka vyombo vya habari kufuatilia kwa umakini taarifa zinazohusu masuala ya kiusalama ili kutoa taarifa sahihi kwa wananchi.
Rai hiyo imetolewa jana jijini Dar es salaam na kaimu msemaji wa jeshi hilo Meja JOSEPH MASANJA wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya vifo vya Askari wawili wa –JWTZ- waliofariki nchini Congo wakiwa katika jukumu la kulinda Amani nchini humo Mei 5 mwaka huu.
MEJA MASANJA amesema kuwa vifo hivyo vimesababishwa na shambulizi lililofanywa na kikundi kilichodhaniwa kuwa ni waasi wa Allied Democratic Force-ADF-kwa kutumia silaha za kivita hali iliyosababisha Askari wawili kupoteza maisha papo hapo.